IOM yaisaidia Ufilipino kukabiliana na mafuriko

20 Agosti 2013

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limeitikia ombi kutoka kwa serikali ya Ufilipino wakati mafuriko makubwa yanapoendelea kuwaathiri zaidi ya watu 600,000  kwenye mji mkuuManila.

Tufani kwa jina Maring na upepo vimezua madhara kwenye nyanda za chini za mji wa Manila pamoja na sehemu zingine za milima kwa muda wa siku tatu zilizopita hali ambayo imesababisha kukwama kwa shughuli nyingi na hata kufungwa kwa biashara, ofisi na shule. Jumbe Omar Jumbe ni afisa wa IOM

 (CLIP YA JUMBE OMARI JUMBE)

 Hadi mapema leo maneo 347  kwenye miji 42 yalikuwa yamefurika huku zaidi ya barabara 60 zikiwa hazipitiki nazo mvua zikitarajiwa kuendelea kunyesha kwa siku mbili au tatu zaidi.