Raia wengi wa Syria wanafurika Kaskazini mwa Iraq.UM

20 Agosti 2013

Idadi ya raia wa Syria wanaokimbia nchini mwao na kumiminika nchiniIraq inazidi kuongezeka kila uchwao ambapo tangu Alhamisi iliyopita, idadi yao imefikia Elfu Thelathini. Jana peke takribani wasyria Elfu Nne Mia Nane walivuka mpaka na kuingia Kaskazini mwaIraq. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi.

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Wengi wanaovuka mpaka huo ni wale wanaohofia usalama wa maisha yao kutokana na milio ya milipuko inayoendelea kusikika nchiniSyria. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendesha jitihada za utoaji wa misaada ya kibinadamu ili kuwasaidia wakimbizi hao wanaovuka mpaka huo.

Shirika la Mpango w Chakula Duniani WFP linaendesha kampeni ya kukusanya chakula kutoka katika hifadhi yake nchini Iraq ili kukabiliana na tatizo la njaa linaloweza kuwaandama raia hao.

Zoezi la ugawaji wa vyakula pamoja na mahitaji mengine kwa ajili ya wakimbizi hao lilitarajiwa kuanza leo jumanne.

Wakati huo huo shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limesema kuwa kiasi cha watu 4,800  ambao wamevuka mpaka kutoka Syria kuelekea katika eneo la Kudirstan nchini Iraq nusu ya hao ni watoto. Wengi wao wanaripotiwa kuwa chini ya umri wa miaka 12. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF

 (SAUTI YA MARIXIE MERCADO)