Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania kuanza kutimua wahamiaji wasio na vibali

Tanzania kuanza kutimua wahamiaji wasio na vibali

Serikali ya Tanzania leo imetangaza operesheni ya kuwatimua raia wa kigeni waliongia nchini humo kinyume cha sheria, ikiwemo wale waliorejea baada ya kuondoka nchini humo hivi karibuni, kutoka Dar Es salaam, George Njogopa anaarifu zaidi.

 (Taarifa ya George)

Bila kujata tarehe rasmi ya kuanza kwa operesheni hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi pia amewatumia salama za onyo baadhi ya raia hao wa kigeni waliokuwepo nchini kinyume cha sheria ambao awali waliondoka lakini wameanza kurejea tena kimya kimya.

 (Sauti ya Nchimbi)