Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 94,000 waathirika na mafuriko Ufilipino:OCHA

Watu 94,000 waathirika na mafuriko Ufilipino:OCHA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA imesema mvua kubwa za monsoon zilizoambatana na kimbunga Trami kinachojulikana nchini Ufilipino kama Maring imesababisha mafuriko na maporomoko ya udongo katika majimbo 11 na Manila mjini kwenye kisiwa cha Luzon.

Serikali ya Ufilipino kwa mujibu wa OCHA inajikita hivi sasa katika kukabiliana mafuriko hayo na kutoa msaada katika majimbo ya Laguna, Rizal na Cavite kwenye mkoa wa Calabarzon ambayo yanasemekana kuathirika zaidi na mafuriko hayo.

Karibu watu 2,200 wamepata hifadhi kwenye vituo maalumu 19,shule nyingi zimefungwa na kwa jumla watu 94,000 wameathirika na mafuriko hayo.