Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu yasikitishwa na vifo na kushikiliwa watu Misri

Ofisi ya haki za binadamu yasikitishwa na vifo na kushikiliwa watu Misri

Ofisi ya haki za binadamu inasikitishwa na idadi ya vifo vinavyoendelea kutokea Misri na pia kushikiliwa kwa viongozi na wafuasi wa kikundi cha Muslim Brotherhood. Kwa mujibu wa ofisi hiyo wale wote waliowekwa rumande haki zao lazima ziheshimiwe. Ofisi hiyo ya haki za binadamu inautaka uongozi nchini Misri kuruhusu kundi la waangalizi wa haki za binadamu kuingia nchini humo. Balozi wa Misri kwenye baraza la haki za binadamu amekutana na naibu kamishina wa haki za binadamu na kusema mwendesha mashitaka mkuu wa Misri anaanzisha uchunguzi kuhusu mauaji yaliyotokea Cairo. Elizabeth Throssell ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu.

(SAUTI YA ELIZABETH THROSSELL)