Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi nchini Libya

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi nchini Libya

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO Bi Irina Bokova amelaani mauji ya mtangazaji wa televisheni nchini Libya Azzedine Qusad yaliyotokea August 9 mwaka huu na kutaka uchunguzi ufanyike dhidi ya mauaji hayo.

Katika taarifa yake Bi Bokova amezitaka mamlaka kuhakiisha waandishi wa habari wanafanya kazi katika mazingira salama huku akisisitiza kuwa uhuru wa kujieleza na ule wa vyombo vya habari utachangia katika juhudi zaLibyakujenga mustakabli mzuri wa raia baada ya kipindi cha migogoro.

Azzedine Qusad aliyekuwa mtangazaji wa televisheni ya shirika liitwalo independent broadcaster for Lybia Al-Hurra aliuwawa akiwa katika garilakemjini Benghazhi baada ya kufyatuliwa risasi na watu watatu ambao hawajafahamika. Mauaji hayo yametokea baada ya waandishi wengine wawili  kushambuliwa siku za hivi karibuni.