Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CERF yatoa dola milioni 10 kwa misaada ya kibinadamu nchini Pakistan

CERF yatoa dola milioni 10 kwa misaada ya kibinadamu nchini Pakistan

Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa CERF umetenga kiasi cha dola milioni 10 kugharamia huduma za kibinadamu kwa zaidi ya watu milioni moja wasio na makao eneo la Khyber Pakhtunkhwa na sehemu za makabila nchini Pakistan kutokana na kuwepo ukosefu wa usalama tangu mwaka 2008. Jason Nyakundi na maelezo kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Fedha hizo zitagharamia misaada cha chakula cha kuokoa maisha, maji ,huduma za usafi kwa watu 900,000 na hudma za fya za dharura kwa watu 350,000 pamoja na za lishe kwa watu 39,000 wakiwemo watoto walio na utapiamlo. Fedha hizo pia zitayawezesha mashirika husika kutoa makao ya dharura na bidhaa zisizokuwa chakula kuwahakikishia usalama na elimu waathiriwa. Hata baada ya kuwepo ukosefu wa misaada zaidi ya watu milioni moja kaskazini mashariki mwa Pakistan wanaendelea kupokea misada ya kibinadamu katoka kwa mashirika tofauti . Mratibu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na huduma za kibinadamu nchini Pakistan Timo Pakkala anasema kuwa mchango huo wa CERF umekuja wakati unaofaa kuweza kuwasaidaia watu wanaohuhitaji.