Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maisha ya wafanyakazi wa misaada yaendelea kuwa hatarini: WFP

Maisha ya wafanyakazi wa misaada yaendelea kuwa hatarini: WFP

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP limetumia siku ya leo kukumbuka watu 22 waliopoteza maisha baada ya ofisi za umoja wa mataifa kushambuliwa hukoBaghdad,Iraq, ambapo WFP yasema miaka kumi baada ya tukiohilobado wafanyakazi wa misaada wanaendelea kuuawa wakitekeleza jukumu la kuokoa maisha yaw engine. George Njogopa na taarifa kamili.

(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Wakati Umoja wa Mataifa ukiadhimisha siku hii ya misaada ya kiutu duniani, Shirika lake linalohusika na mpango wa chakula duniani WFP,linawakumbuka watumishi wake wapatao kumi ambao walikumbwa na umauti miaka 10 iliyopita wakati wakitekeleza majukumu ya kiutu katika nchi za Rwanda, Sudan , Sudan Kuisn na huko Afghanistan.

Katika taarifa yake, WFP dunia itaendelea kuwakumbuka na kuwapa heshima zote kutokana na ujasiri wao wa kukubali kutumika katika mazingira ya hatari ili kukabiliana na janga la njaa.

Pia WFP imetumia siku hii kutuma salama za heshimu kwa watumishi wengine ambao nao pia wamekabiliana na matukio mbalimbali wakati wakitekeleza majukumuyaoya usamaria mwema.

Taarifa hiyo ya WFP imesema dunia haipaswi kukaa kando na kuacha jukumu la kuwakirimu wale wenye matatizo ya njaa likaachwa lifanywe na wachache bali inawajibu wa kutoa msaada wa hali na mali ili kufanikisha agenda ya pamoja na kupiga vita umaskini, njaa na vikwazo vya maendeleo.