Jopo la UM la kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali Syria, lawasili Damascus

18 Agosti 2013

Ofisi ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imearifu ya kwamba jopo lililoundwa na Katibu Mkuu Ban Ki Moon kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria limewasili mjini Damascus Jumapili. Jopo hilo linaloongozwa na Profesa Ǻke Sellström, litaanza kazi yake Jumatatu tarehe 19. kwa mujibu wa taarifa ya leo, maelezo zaidi yatakuwa yanatolewa mjini New York kadri taarifa zitakavyokuwa zikipatikana. Tarehe 15 mwezi huu wa Agosti, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alitangaza kuwa serikali ya Syria  imekubali rasmi kutoa ushirikiano kuwezesha timu ya waangalizi kuendesha majukumu yake katika mazingira safi, salama na katika hali ya ufanisi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter