Changamoto ya kukosa ajira iliibua fursa ya kujiajiri jijini Nairobi:
Wiki mbili za mwanzo wa mwezi huu wa Agosti, kumefanyika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana, na kwingineko madhimisho hayo yanaendelea kwa ngazi ya kitaifa. Kubwa lililokuwa linamulikwa ni jinsi vijana wanahaha kuhama vijiji, mikoa na hata nchi zao kusaka ajira bora ali mradi mkono uende kinywani. Umoja wa Mataifa unasema kuwa hali ngumu ya kiuchumi, mizozo ya kijamii ikiwemo ndani ya familia ni moja ya sababu za vijana kuhama sehemu moja kwenda nyingine. Lakini bado wengine wanaamua kuwa licha ya mazingira ni lazima wafungue machoyaozaidi na kupata fursa za kujiajiri kwani penye changamoto yoyote ile hapakosi fursa. Je wanafanyaje? Ungana na Jason Nyakundi katika makala hii ya wiki.