Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukata wakwamisha miradi ya usaidizi wa kibinadamu Korea Kaskazini: OCHA

Ukata wakwamisha miradi ya usaidizi wa kibinadamu Korea Kaskazini: OCHA

Umoja wa Mataifa umesema kuwa miradi mingi inayotekelezwa na taasisi zake tano huko Korea ya Kaskazini, DPRK,  bado haijapata ufadhili wa kutosha. Umesema kuna hitajio la dharura za dola za Marekani milioni 90 ambazo ni kati ya dola milioni 150 zilihitajika kwa ajili ya mwaka 2013. Kiasi hicho cha fedha kinachohitajika kwa haraka ni kwa ajili kuendeleza miradi ya kilimo,  maji, afya na lishe. Jens Laerke kutoka shirika la kuhudumia misaada ya kiutu OCHA anasema kuwa kiasi cha watu milioni 2.4 wapo hatarini kukubwa na tatizo la ukosefu wa chakula hivyo ametaka kuongeza kasi ya kufadhilia miradi iliyobuniwa.