Tanzania kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana Jumamosi

16 Agosti 2013

Nchini Tanzania, Jumamosi ya tarehe 17 mwezi Agosti itakuwa ni kilele cha kitaifa cha siku ya vijana duniani ambapo maadhimisho hayo yatafanyika jijini Dar es salaam na hukoZanzibar. Taarifa ya Assumpta Massoi inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Assumpta)

Ujumbe wa mwaka huu ni uhamiaji wa vijana na kusongesha mbele maendeleo ambapo Naibu Mkurugenzi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Venerosa Mtenga amaesema ni dhahiri shahiri kuwa uhamiaji una manufaa lakini pia una changamoto zake ambazo wakati wa maadhimisho hayo ndiyo zitamulikwa zaidi.  

(SAUTI YA VENEROSA)

 Afisa vijana kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, UNFPA Uduak Bassey amewaambia waandishi wa habari kuwa pamoja na kutoa fursa kwa vijana kupima afya zao kama vile virusi vya Ukimwi wakati wa sherehe hizo zitakazofanyika Manzese, pia wanatafuta mchoro bora unaoendana na ujumbe wa mwaka huu wa siku ya vijana.

 (Sauti  ya Uduak)

 

“Shule ambazo tumeenda tumewapatia taarifa za juu ya nini kuandaa na hadi sasa tumeshapokea kazi za sanaa kutoka kwa vijana na hizo zitaonyeshwa Jumamosi.”