Tiba endelevu ya afya ya akili kwa wahanga wa ghasia ni muhimu: WHO

16 Agosti 2013

Katika kuelekea siku ya kimataifa ya usaidizi wa kibinadamu tarehe 19 mwezi huu, shirika la afya duniani WHO limetoa wito kwa tiba endelevu dhidi ya magonjwa ya akili kupatiwa kipaumbele hususan kwenye maeneo ya migogoro.

Ripoti mpya ya WHO kuhusu huduma ya afya ya akili baada ya dharura, inasema mashirika ya misaada huwa yanahaha kutoa usadizi wa tiba ya magonjwa ya akili kwa manusura wa ghasia lakini jitihada hizo huingia kapuni kwa kuwa hakuna mifumo endelevu ya kuendeleza kile kinachoanzishwa na mashirika hayo. Dkt. Mark Van Ommeren kutoka Idara ya Afya ya akili na matumizi ya madawa ya kulevya ndani ya WHO anasema ijapokuwa mazingira ya dharura yanatisha, lakini huwa ni fursa ya kuboresha huduma za afya ya akili lakini kuna walakini kuhusu mwendelezo wake.

(Sauti ya Dr Mark Van Ommeren)

Kwa mantiki hiyo ripoti inatoa mwongozo wa kuimarisha mifumo ya afya hususan ya akili baada ya migogoro ikitolea mfano Burundi, Somali na Sri Lanka.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter