Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Arancha Gonzalez wa Uhispania kama Mkuu wa ITC

Ban amteua Arancha Gonzalez wa Uhispania kama Mkuu wa ITC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Arancha Gonzalez wa Uhispania kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Biashara, ITC, ambacho huwakilisha Kamati ya Biashara na Maendeleo katika Umoja wa Mataifa, UNCTAD na Shirika la Biashara Duniani, WTO katika  maendeleo ya kimataifa biashara.

Bi Gonzalez atamrithi Patricia Francis wa Jamaica, ambaye amepongezwa na Bwana Ban kwa huduma yake ya kujitoa kwa Umoja wa Mataifa.

Bi Gonzalez ana uzoefu mkubwa wa kuhudumu katika sekta ya umma na sekta ya kibinafsi, akiwa amehudumu katika WTO kama msimamizi wa wafanyakazi na kama msemaji wa masuala ya biashara katika jumuiya ya nchi za Ulaya, EU.