Skip to main content

Utafiti wa kiafya ndio njia ya pekee ya kuhakikisha kila moja amepata huduma:WHO

Utafiti wa kiafya ndio njia ya pekee ya kuhakikisha kila moja amepata huduma:WHO

Shirika la afya duniani WHO linazitaka nchi kuwekeza kwenye utafiti wa kimataifa wa kubuniwa kwa bima ya afya kwa kila mmoja na kwa kila nchi kote duniani. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Jason)

WHO inasema kuwa kupitya kwa bima ya afya nchi zinaweza kuhakikisha kuwa wananchi wamapata huduma za afya wanazohitaji bila kuhangaishwa na ugumu wa kuzilipia. Akiongea mjini Beijing nchini China wakati wa uzinduzi wa ripoti ya afya duniani ya mwaka 2013 mkurugenzi mkuuwa WHO Dr Margaret Chan anasema kuwa bima ya afya ndiyo njia bora katika kuhakikisha kuna usawa kwenye utoaji wa huduma za afya. Ripoti hiyo inaonyesha jinsi mataifa kwa kutumia bima ya afya yanaweza kutumia utafiti kubaini ni masuala yapi yanayohitaji kushughulikiwa na jinsi ya kubaini maendeleo ya kiafya

(SAUTI ya Dr Christopher Dye ni kutoka ofisi ya habari ya WHO)