Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu lakutana kujadili Ushirikiano Mpya kwa Maendeleo ya Afrika, NEPAD

Baraza Kuu lakutana kujadili Ushirikiano Mpya kwa Maendeleo ya Afrika, NEPAD

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo limefanya kikao ambacho kimeangazia utekelezaji wa ushirikiano mpya wa maendeleo barani Afrika. Joshua Mmali ameufuatilia mkutano huo

(TAARIFA YA JOSHUA MMALI)

Katika kikao cha leo, wanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wamepitisha kwa kauli moja azimio kuhusu ushirikiano mpya wa maendeleo barani Afrika, NEPAD, na ambalo linaangazia hatua zilizopigwa na uungwaji mkono wa jamii ya kimataifa katika kuutekeleza ushirikiano huo.

Akiliwasilisha mswada wa azimio hilo kwa niaba ya Uchina na Kundi la Mataifa 77, Mwakilishi wa taifa la Fiji Peter Thomson, amesema NEPAD imeweka mfumo bora wa kuendeleza sera mikakati mbalimbali kama vile ile ya maendeleo ya kilimo na miundo mbinu.

(SAUTI YA THOMSON)

Azimio hilo pia linaunga mkono juhudi za nchi za Afrika kushirikiana katika kuweka ajenda za maendeleo na kuwahusisha wanawake katika kutekeleza ushirikiano huo mpya.