Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakulima wapata ugumu kuendesha mbinu zinazoendana vyema na tabianchi: FAO

Wakulima wapata ugumu kuendesha mbinu zinazoendana vyema na tabianchi: FAO

Matokeo ya awali ya mradi ulonuiwa kusaidia nchi za Malawi, Vietnam na Zambia kubadili mbinu za ukulima ili zikabiliane vyema na mabadiliko ya tabianchi, zinaonyesha kuwa baadhi ya wakulima wanapata ugumu kuendesha mbinu hizo mpya.

Licha ya hayo, mradi huo pia umebainisha wakulima ambao wanabuni njia nzuri za kukabiliana na matatizo ya tabianchi kama vile kuchelewa kwa misimu ya mvua. Ripoti ya Alice Kariuki inafafanua zaidi.

(Taarifa ya Alice)

Mradi huo uliozinduliwa mwezi Januari mwaka 2012 kwa gharama ya Uro milioni 5.3 utahakikisha kuwepo kwa kilimo kisichoathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa kwenye kila nchi. Shughuli muhimu kwenye mradi huo ni kutambua ni mbinu zipi za kilimo ambazo zinaweza kustahimili makadiliko ya hali ya hewa. Mbinu hizi zimepata uungwaji mkono nchini Malawi na Zambia. Hata hivyo tathmini inaonyesha kuwa wakulima wengi kwenye nchi hizo mbili wana ugumu wa kutumia mbinu hizo kwa kuwa wengi ni maskini zaidi kuweza kuzifuatilia. Mkuu wa kitengo uchumi na sera kwenye Shirika la kilimo na Mazao la Umoja wa Mataifa FAO Leslie Lipper anasema kuwa kuongezwa kwa uwekezaji unaohitajika kutawasaidia wakulima kufanya mabadiliko yanayohitajika.