UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi nchini Guatamala.

14 Agosti 2013

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO , Irina Bukova,  amelaani mauaji ya  mwandishi wa habari mkongwe wa radio huko nchini Guatamala anayeitwa  Luis de JesúsLima.

Katika taarifa yake Bi Bukova ameitaka mamlaka nchini humo kufanya kila liwezekanalo kuwafikisha wahusika wa mauaji hayo katika vyombo vya sheria akisema kutoshughulikia ukatili dhidi ya waandishi wa habari ni kutoitendea haki tasnia hiyo jambo linaloshushia hadhi uhuru wa kujieleza na kupata taarifa.

Lima aliyekuwa na umri wa mika 68 alipigwa risasi August 6 alipokuwa akiwasili kwenye kituo chake cha kazi  katika Radio Sultana Zacapata, ambapo alikuwa akiendesha kipindi mashuhuri cha muziki kilichojumuisha mahojiano na watu wa kawaida .

Anakuwa mwandishi wa tatu kuuwawa nchini humo kwa mwaka huu pekee.