Naibu Katibu Mkuu asema ripoti ya huduma ya usafi na maji safi na salama kwa wote inatia moyo

14 Agosti 2013

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amepongeza hatua zilizofikiwa katika kuhakikisha kila mkazi wa dunia anapata huduma ya majisafina salama bila kusahau matumizi ya vyoo kwa ajili ya kuweka mazingirasafi. Ametoa pongeza hizo kufuatia ripoti ya maendeleo ya kufanikisha hali hiyo iliyotolewa leo mjiniGeneva, Uswisi na jopo la ngazi ya juu lililoundwa mwaka 2012. Bwana Eliasson amesema ripoti hiyo inatia moyo kwa kuwa utashi wa kisiasa uko dhahiri kwani serikali zinaonekana kuongeza bajeti na hata kuimarisha mipango ya kitaifa ya kuhakikisha huduma hizo zinapatikana pamoja na kupungua kwa watu wasiokuwa na vyoo. Hata hivyo amesema changamoto hivi sasa ni kuendeleza kasi hiyo na kutokomeza vikwazo vya kutekeleza ahadi zilizotolewa. Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu, mwezi Aprili mwakani, jopo hilo linalohusika na huduma za maji safi na salama pamoja na usari kwa wote, litakuwa na kikao cha ngazi ya juu na amesema ni matumaini yake kuwa mashauriano yatakuwa ni ya dhati ili ndoto ya kuwa na huduma hiyo iweze kutimia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud