Mfuko wa majanga ya dharura wa UM waidhinisha msaada wa fedha kwa Sudan Kusini

14 Agosti 2013

Mfuko wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya dharura umeidhinisha dola Milioni Sita kwa ajili ya kusaidia mashirika ya misaada yanayosambaza huduma za chakula na mahitaji mengine nchini Sudan Kusini. Msaada huo ambayo pia inahusisha huduma ya majisafina salama unawalenga mamia ya wananchi walioathiriwa na machafuko katika eneo la Pibor kwenye Jimbo la Jonglei . Taarifa zaidi na Alice Kariuki:

 (Taarifa ya Alice)

Mfuko huo wa kukabili majanga ya dharura umesema kuwa kiasi hicho cha fedha ni ongezeko la dola Mlioni Tano nukta Tano ambacho kiliidhinishwa mwezi Juni mwaka huu kwa ajili ya ufanikishaji kusambaza misaada ya kiutu. Mratibu wa shughuli za misaada ya kiutu huko Sudan Kusini Toby Lanzer,amesema kuwa ametiwa moyo namna mashirika ya kutoa misaada yanavyotambua hali ngumu iliyopo katika jimbohilohivyo kuidhinishwa kwa fedha hizo kutasaidia kukwamua watu wanaoishi kwenye eneohilo.

Amesema kuwa fedha hizo zitasaidia kuwafikia zaidi ya watu 60,000 ambao wanaandamwa na matatizo mbalimbali ikiwemo mahitaji ya chakula. Kutolewa kwa msaada huo wa fedha kunakuja katika wakati ambapo Sudan Kusini ikiwa imesaidia kwa asilimia 60 katika mpango wake wa awali uliohitaji msaada wa fedha ili kuendesha miradi yake mbalimbali.