Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Haoliang Xu wa Uchina kama Msimamizi Msaidizi wa UNDP

Ban amteua Haoliang Xu wa Uchina kama Msimamizi Msaidizi wa UNDP

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Bwana Haoliang Xu wa Uchina kama Msimamizi Msaidizi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo katika Umoja wa Mataifa, UNDP na Mkurugenzi wa Ofisi ya UNDP bara Asia na Pasifiki.

Bwana Xu atairithi nafasi ya Ajay Chhibber wa India, ambaye amemsifu kwa huduma yake ya kujitoa kwa Umoja wa Mataifa akiwa UNDP.

Bwana Xu ana uzoefu wa miaka mingi ya kuhudumu katika UNDP, ambako ameshikilia nyadhfa mbalimbali za uongozi, zikiwemo kama Mratibu Mkaazi Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkaazi wa UNDP nchini Kazakhstan, Mkurugezi wa UNDP nchini Pakistan, na pia kuhudumu katika nchi za Timor-Leste na Iran.