Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mapigano mapya yaripotiwa Mynamar

Mapigano mapya yaripotiwa Mynamar

Kumekuwa na taarifa ya kuzuka machafuko baina ya kundi la waislamu waliokosa makazi na vikosi vya serikali katika jimbo la Rakhine nchini Mynmar.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema kuwa mapigano hayo yaliyotokea mwishoni mwa juma, yamesababisha kifo cha mtu mmoja na wengine 10 wamejeruhiwa.

UNHCR imerejelea mwito wake kwa kuzitaka pande zinazohitilafiana kwenye eneo hilo kusaka suluhu ya majadiliano ya mezani.

Watu zaidi  140,000 hawana makazi hadi sasa katika jimbo hilo  kutokana na machafuko ya mara kwa mara.

Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR

(Sauti ya Adrian)