UNICEF yaanza kutoa huduma za afya CAR, lakini hali bado ni mbaya

13 Agosti 2013

Hali ya huduma za kibinamu katika Jamhuri ya Afrika Kati imeendelea kuwa tete katika wakati  ambapo shughuli za usambazaji wa huduma za usamaria zikikatizwa kutokana  na kuzorota kwa usamala.

Hata hivyo shirika la kudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema kuwa limefaulu kwa kiasi kidogo kuimarisha upya vituo vya afya vilivyopo katika wilaya mbili zilizoko katika eneo la katika ya nchi  ambako kumeathiriwa vibaya na machafuko ya hivi karibuni

George Njogopa na taarifa zaidi:

(Taarifa ya George)

Vituo hivyo ambavyo zinaweza kusafirishwa sehemu moja hadi nyingine ambavyo vimesimikwa katika wilaya za Kaga, Bandoro na Bambari zinauwezo wa kuhudumia watu wanaokadiriwa kufikia166,000. Baada ya kusita kutoa huduma kwa kipindi kirefu vituo hivyo vimesambaziwa vifaa kadhaa na tayari vimeanza kuchapa kazi. Marixie Mercado kutoka  UNICEF anasema kuwa mipango iliyopo ni kusambaza huduma hiyo katika maeneo mengine zaidi ili kuwafikia zaidi ya watu 325,000 katika kipindi cha siku chache zijazo.

(SAUTI YA MARIXIE)

“Kupitia mpango huu w adharura na katika maeneo mengine ya nchi nzima,UNICEF inafanya kazi na mamlaka za serikali na wahisani wengine kuzirejesha upya huduma za msingi za kiafya mahala popote pale ambako hali ya usalama inaruhusu.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, tulifanikiwa kuleta kiasi cha tani 50 cha huduma za usamaria mwema.

Kampeni za kutoa chanjo zilizoanzishwa nchini humu zimefanikiwa kuwafikia zaidi ya watoto200,000 tangu mwezi May, na mkazo ni kutoa chanjo dhidi ya magonjwa ya surua na polio na ikiwemo pia vitamin A."

UNICEF pia imetoa wito wa kuongezwa misaada ya kiutu ili kufanikusha operesheni yake nchini humo ikisema kuwa hadi sasa imepokea kiasi cha dola za Marekani milioni 9, kati 32.4 ilizoomba