Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wataka hakikisho la usalama wa mwanaharakati Adilur huko Bangladesh

UM wataka hakikisho la usalama wa mwanaharakati Adilur huko Bangladesh

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeeleza wasiwasi wake juu ya kukamatwa kwa mwanaharakati mashuhuri nchiniBangladesh, Adilur Rahman Khan mwishoni mwa wiki. Habari zinasema Adilur ambaye ni Mkurugenzi wa kikundi cha Odhikar, alikamatwa na maafisa wa usalama kwenye mji mkuuDhakabila ya kuwa na kibali cha kumkamata. Mwanaharakati huyo anatuhumiwa kuchapisha taarifa zisizo sahihi kuhusiana na maandamano ya hivi karibuni yaliyodaiwa kuwa na ghasia. Elizabeth Throssell ni msemaji wa Ofisi ya Haki za binadamu  ya Umoja wa Mataifa.

 (Sauti ya Throssell)

 Odhika wameripoti kuwa watu 61 walikufa wakati wa maandamano, tofauti na ripoti ya serikali juu ya tukio hilo. Tarehe 11 mwezi Agosti, Bwana Khan alinyimwa dhamana na kutakiwa kubaki rumande kwa siku Tano. Inadaiwa alinyimwa kuonana na wakili kabla ya kufikishwa mahakamani. Tunaitaka serikali ya Bangladesh kuhakikisha utu wa kifikra na kisaikolojia wa Bwana Khan ambaye kukamatwa kwake kunaweza kuhusishwa na kazi yake ya utetezi wa haki za binadamu.”