Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Peter de Clercq wa Uholanzi kuwa Naibu Msaidizi maalum Haiti

Ban amteua Peter de Clercq wa Uholanzi kuwa Naibu Msaidizi maalum Haiti

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Bwana Peter de Clercq wa Uholanzi kuwa Naibu Msaidizi wake maalum katika Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, MINUSTAH, ambako pia atahudumu kama Mratibu Mkaazi wa Umoja wa Mataifa, Mratibu wa misaada ya kibinadamu na Mwakilishi Mkaazi.

Bwana de Clercq atamrithi Bwana Nigel Fisher wa Canada, ambaye amehitimisha uteuzi wake mwezi Julai mwaka huu 2013. Katibu Mkuu amemsifu Bwana Fisher kwa huduma yake ya umakinifu nchini Haiti, ikiwemo kama Mwakilishi maalum wa muda kuanzia Februari 2013.

Bwana de Clercq ambaye sasa ni Mshauri Mkuu wa Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia na Mkuu wa UNSOM, aliwahi kuhudumu kama Naibu Mwakilishi maalum Augustine Mahiga, ambaye alikuwa mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kisiasa kuhusu Somalia, UNPOS.