Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MINUSMA yasaidia usafirishaji wa nyaraka za matokeo ya uchaguzi Mali

MINUSMA yasaidia usafirishaji wa nyaraka za matokeo ya uchaguzi Mali

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kusimamia kurejea kwa utulivu nchini Mali, MINUSMA inasaidia mamlaka za uchaguzi nchini humo kuharakisha mchakato wa kuhesabu kura kufuatia awamu ya pili ya uchaguzi iliyofanyika Jumapili. MINUSMA imesema kuwa hakuna jambo kubwa lililojitokeza wakati wa upigaji kura ingawa mvua kubwa zilikwamisha kwa kiasi fulani upigaji kura kwenye sehemu nyingi nchiniMali. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Msemaji wa Umoja wa Mataifa Eduardo Del Buey alipozungumza na waandishi wa habari mjiniNew York, Marekani.

(SAUTI YA DEL BUEY)

"Kwa mujibu wa mamlaka yake, MINUSMA imetoa misaada ya kiufundi na vifaa kwa awamu zote mbili za uchaguzi pamoja na kusaidia mamlaka za ulinzi. Katika kuharakisha mchakato wa kuhesabu kura, MINUSMA kwa kutumia ndege inasaidia mamlaka za uchaguzi n chini Mali kurejesha nyaraka za matokeo ya uchaguzi huo kutoka Gao, Timbuktu na Kidal.”

Awamu ya kwanza ya uchaguzi wa Rais nchiniMaliilifanyika tarehe 28 mwezi uliopita ikiwa ni jitihada za kumaliza mgogoro wa kisiasa ulioanza mwaka jana baada ya askari kupindua serikali. Mgogoro huo ulisababisha kuibuka kwa mapigano kati ya majeshi ya serikali na vikosi vya waasi wa Tuareg na sehemu ya kaskazini mwaMalikushikiliwa na waislamu wenye msimamo mkali.