Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji vijana bado wanafanya kazi zisizo na hadhi: ILO

Wahamiaji vijana bado wanafanya kazi zisizo na hadhi: ILO

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya vijana hii leo, shirika la kazi duniani, ILO limemulika ujumbe wa siku hii kuhusu vijana na uhamiaji na kusema kuwa idadi kubwa ya vijana wanaohama nchi zao kwenda kusaka maisha bora ughaibuni hutumbukia kwenye ajira zisizo na hadhi, za mateso huku wakipata ujira mdogo.  Mkurugenzi Mkuu wa ILO Guy Ryder katika ujumbe wake amesema kati ya wahamiaji Milioni 214 duniani kote, Milioni 27 ni vijana lakini wengi wao hujikuta wakitumikishwa kazi na huwa visingizio vya matatizo ya kiuchumi na kijamii yanayokumba mataifa mbali mbali duniani. Bwana Ryder amesema pamoja na kutambua mchango wao katika maendeleo ya nchi, ni lazima hatua za makusudi zichukuliwe ili kuimarisha usalama wao wafanyakazi wahamiaji vijana na kuheshimu haki na utu wao. Mathalani amesema nchi ambazo vijana hao wanatoka wanaweza kupatiwa stadi na taarifa kuhusu ajira kule wanakoelekea na nchi ambamo wanakwenda wapatiwe fursa sawakamawafanyakazi wengine.