Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO yazindua chombo cha kisasa kukusanya takwimu za misitu nchini Uganda

FAO yazindua chombo cha kisasa kukusanya takwimu za misitu nchini Uganda

Shirika la Chakula na Kilimo duniani, FAO limeanzisha utaratibu mpya nchini Uganda ambao utaiwezesha nchi hiyo kuwa na takwimu sahihi kuhusiana na mazao ya misitu na ardhi. FAO imezindua teknolojia ramani ambayo inatajwa kuwa mkombozi waUgandakutokana na wananchi wake wengi kutegemea mazao yatokanayo ya msitu. Alice Kariuki na taarifa kamili.  

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI) 

Teknolojia hiyo mpya inatoa fursa kwa serikali kufuatilia kwa karibu rasilimali za taifa ikiwemo misitu. Kuwepo kwa hatua hiyo pia kunatazamia kutoa tija kubwa wakati wa upitishwaji uamuzi kuhusu miradi ya muda mrefu.  Wataalamu wanasema kuwepo kwa teknolojia hiyo kutaisaidiaUgandakutojiingiza kwenye miradi ya uwekezaji ambayo inaweza kusababisha matatizo ya kimazingira. Ubunifu huo wa FAO unaelezwa kuwa rafiki kutokana na kutohitaji fedha nyingi wakati wa utekelezaji wa miradi ya uwekezaji. Takwimu zitakazokusanywa kupitia chombo hicho kipya, zitatumiwa na FAO kupitia chapisho lake litakalotoka mwaka 2015 kuelezea rasilimali za misitu.