Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mitandao ya kijamii yachochoea kwa kasi kuenea kwa hotuba za chuki ya misingi ya ubaguzi wa rangi : UM

Mitandao ya kijamii yachochoea kwa kasi kuenea kwa hotuba za chuki ya misingi ya ubaguzi wa rangi : UM

Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, imeonyesha wasiwasi wake juu ya kasi kubwa hivi sasa ya ambamo kwayo mitandao ya kijamii pamoja na intaneti inasambaza hotuba zenye chuki ya misingi ya ubaguzi wa rangi. Joseph Msami na taarifa kamili.

(Taarifa ya Joseph Msami)

Akizungumza mwanzoni mwa kikao cha 83 cha kamati ya kutokomeza ubaguzi kwa misingi ya rangi hukoGeneva, Uswisi, Naibu Kamishna wa Tume ya Haki za  binadamu Flavia Pansieri amesema hali hiyo inatokana na ukosefu wa ainisho linalokubalika dunia nzima juu ya hotuba zenye chuki. Amesema kujumuisha elimu ya  haki za binadamu kwenye shule kutawezesha hatimaye kuzuia na kutokomeza aina zote za ubaguzi kwa misingi ya rangi na hata kutokuvumiliana. Ametaka kamati hiyo kuchunguza na kuibuka na mikakati sahihi ya kudhibiti hali hiyo ikiwa ni pamoja na ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Albino.

(SAUTI YA Pansieri)

“Wapi ambapo haki ya kujieleza ambayo sote tunaitaka inakomea na umuhimu wa kuweka vikwazo ili kuzuia hotuba za chuki ianzie? Ni wakati gani ambapo wajibu wa mtu kupaswa kutambua kuwa haki yake haiweze kutekelezwa iwapo inakiuka haki ya mwingine? Maalbino wamekuwa wakichukiwa waziwazi. Kati nchi 15 za Afrika wamekuwa wakitekwa na mtaalamu maalum ametaka serikali zihamamishe watu kutambua kuwa rangi tofauti ya albino haimfanyi yeye kutokuwa binadamu kamilifu na kumkosesha haki ya kupata haki zote za kuheshimiwa na kulindwa.”

Katika kikao hicho, Kamati hiyo itaangalia ripoti kutoka Chile, Chad, Venezuela, Burkina Faso, Belarus, Jamaica, Sweden na Cyprus.