Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya watu asili yaadhimishwa Burundi

Siku ya watu asili yaadhimishwa Burundi

Agosti 9 ulimwengu huadhimisha siku ya kimataifa ya watu asili. Watu hao wamekuwa wanakumbana na changamoto nyingi za kuwa staawisha katika jamii wanamoishi na kukubalika kama wananchi katika mataifa yao asili. Moja mwa sehemu ambako wanashuhudiwa kwa wingi watu hao asili ni katika eneo la maziwa makuu.Wawakilishi wa jamii hizo za watu asili wamekutana wiki hii mjini Bujumbura kupaza sauti kushinikiza uwakilishi katika taasisi za maongozi ya taifa, kama sehemu ya jitihada ya kutaka kusikilizwa kero zao.

Ili kujua mengi zaidi kuhusiana na watu hao asili, Muandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani KIBUGA ametuandalia makala haya akiwa mjini Bujumbura. Karibu ungana naye.