Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajali ya ndege Somalia, Muungano wa Afrika watuma rambirambi

Ajali ya ndege Somalia, Muungano wa Afrika watuma rambirambi

taarifamaalumajalisomalia-13Watu wanne wameripotiwa kuaga dunia baada ya ndege ya jeshi laEthiopiakuangkua ilipokuwa ikitua kwenye uwanja wa ndege mjini Mogadishi nchiniSomalia.

Watu wengine wawili walijeruhiwa kwenye ajali hiyo amabapoi naripotiwa kuwa ndege hiyo ilishika moto mara baada ya kuanguka lakini wazima moto waliokuwa karibuni wakaizima na kuwaokoa manusura wawili.

Kile ambacho kilisababisha kuanguka kwa ndege hiyo bado hakijabainika. Mjumbe maalum na mwenyekiti wa ujumbe wa tume ya Muunfano wa Afrika nchini Somalia balozi Mahamat Saleh Annadif ametuma rambi rambi zake kwa serikali na kwa watu wa Ethiopia kwa wale waliowapoteza wapendwa wao na kuwatakia nafuu waliojeruhiwa.