Colombia ilizalisha kiwango kidogo cha coka msimu wa mwaka 2012-Ripoti ya UM

9 Agosti 2013

Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kuhusiana na uzalishaji wa zao za Coca nchini Colombia ikiwa ni moja ya nchi zinazozalisha kwa wingi duniani, inaonyesha kuporomoka katika msimu wa mwaka 2012. Zao hilo ambalo pia huzalishwa kwa wingi katika nchi za Bolivia na Peru lilianguka kwa kiwango cha robo tatu kama ilivyobainishwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifu. Ripoti hiyo imesema kuwa kumekuwa na anguka la hekari 48,000 ikiwa imeshuka kutoka hekali 64,000 zilizorekodiwa katika msimu wa mwaka 2011. Kulingana na picha za seteliti, baadhi ya maeneo bado yameendelea kushika kasi kwa kuzalisha kwa wingi mmeo huo ambao serikali ya Colombia imekuwa ikiendesha juhudi za kuundosha.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter