Saudi Arabia yatoa mchango wake kwa jitihada za kupambana na ugaidi kwa UM

9 Agosti 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon ametoa shukran zake nyingi zake kwa mfalme Abdullah bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia kwa mchango wake wa dola milioni 100 kwa jitihada za Umoja nwa Mataifa za kupambana na ugaidi. Kama mmoja wa waanzishaji wa Umoja wa Mataifa taifa la Saudi Arabia limeunga mkono jitihada za Umoja wa Mataifa kote duniani katika nyanja tofauti.

Amesema kuwa mchango wa hivi punde utauwezesha umoja wa amataifa kuzisaidia nchi kupambana na tatizo la ugaidi kuambatana na mpango ulioafikiwa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2006. Katibu mkuu ameahida ushirikino wa kuendelea kufanya kazi na nchi zote wanachama kupitia kwa mashirika ya kupambana na ugaidi ili kuboresha jitihada za kimataifa za kukabiliana na ugaidi wa kimataifa.