Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mikataba ya kutetea haki za watu wa asili yamulikwa

Mikataba ya kutetea haki za watu wa asili yamulikwa

“Tunapaswa kushirikiana kuimarisha ubia na kuhakikisha sera na vitendo vyovyote tunavyofanya vinaakisi maadili ya watu wa asili”, ni kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watu wa asili hii leo. Bwana Ban amesema watu wa asili wanawakilisha zaidi ya makundi tofauti Elfu Tano duniani kote ambao ni takribani asilimia Tano ya wakazi wa dunia hii na kwamba ni vyema kumulika mikataba yote iliyoidhinishwa hata na waasisi waliotangulia ili kuendeleza maadili yao kwa maslahi ya dunia. Ujumbe wa mwaka huu ni kuheshimu mikataba kuhusu watu wa asili ukimulikwa ule uliotiwa saini miaka 400 kati ya wadachi na wahamiaji Haudenosaunee.  Paul Kanyike Sena ni Mwenyekiti wa mkutano wa kudumu unaohusika na masuala ya watu wa asili.

 (SAUTI YA PAUL KANYIKE)

 Takwimu zinaonyesha kuwepo kwa watu Milioni 370 wa asili kwenye mataifa 90 wakiendeleza mila, desturi na shughuli za kiuchumi na kijamii tofauti na vile vinavyotekelezwa na jamii ambamo wanaishi.