Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban azungumza na Rais Kiir wa Sudan Kusini

Ban azungumza na Rais Kiir wa Sudan Kusini

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo na Rais Salva Kiir waSudanKusini ambapo amemweleza kuwa amekuwa akifuatilia hali ilivyo nchini humo na kwamba hali ya utulivu imerejea baada ya mabadiliko ya baraza la mawaziri. Katika mazungumzo hayo kwa njia ya simu Bwana Ban pia amezungumzia azma ya Umoja wa Mataifa ya kuendelea kufanya kazi pamoja na serikali ikiwemo mawaziri wapya pindi watakapoapishwa. Hata hivyo Katibu Mkuu ameelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya hali ya usalama inavyozorota kwenye jimbo la Jonglei na kutaka serikali ya Sudan kusini ikiwemo jeshi la nchi hiyo kuhakikisha usalama na ulinzi wa raia. Halikadhalika amekumbusha azma ya Rais Kiir ya kuhakikisha yeyote anayehusika na matukio hayo anawajibishwa. Kuhusu masuala ya Sudan Kusini naSudan, Katibu Mkuu amesema ametiwa moyo na uamuzi wa serikali yaSudanwa kuahirisha siku ya mwisho ya kufunga bomba linalosafirisha mafuta kutoka Sudan Kusini hadi tarehe 21 mwezi huu.