Dhana ya kwamba vyakula vya mikebe ni bora kuliko kunyonyesha inapotosha:WHO

8 Agosti 2013

Agosti Mosi hadi Saba ni wiki ya unyonyeshaji duniani. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, maziwa ya mama ndicho chanzo bora zaidi cha lishe kwa watoto wabembe na watoto kwa ujumla. Ingawa karibu akina mama wote wana uwezo wa kunyonyesha, WHO inasema wengi wao hawafanyi hivyo kwa sababu wanapotoshwa na kuamini kuwa vyakula vya mikebe ni bora zaidi kwa watoto wao.

Katika ripoti ya utafiti wa WHO ambayo imetolewa kwa ajili ya wiki ya kunyonyesha duniani ambayo imehitimishwa hapo jana, inaonyesha kuwa ni nchi chache tu ambazo hutekeleza mfumo wa kimataifa, unaolenga kuzuia matangazo ya lishe mbadala kwa watoto, ambayo huwachochea akina mama kutonyonyesha na badala yake kununua na kuwapa watoto wao vyakula vya mikebe.

Ungana basi na Joshua Mmali kwa makala hii maalum inayomulika unyonyeshaji wa watoto katika nchi za Afrika Mashiriki