Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuachiwa kwa wafuasi wa Gbagbo ni hatua njema kuelekea maridhiano ya kitaifa Côte d’Ivoire

Kuachiwa kwa wafuasi wa Gbagbo ni hatua njema kuelekea maridhiano ya kitaifa Côte d’Ivoire

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Côte d’Ivoire Doudou Diène amesema kitendo cha kuachiwa huru kwa wafuasi 14 wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Gbagbo baada ya kuhusishwa na vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi, ni hatua njema kuelekea maridhiano ya kitaifa.Wafuasi hao waliachiwa huru wiki hii na mahakama mjini Abidjan baada ya kuwepo rumande kwa kipindi cha miaka miwili. Akizungumza mjini Geneva, Bwana Diène amesema uamuzi huo unaweza kuchochea kasi kubwa ya mashauriano ya kisiasa na pia ni fursa kwa wananchi kutambua na kukubali madhara makubwa ya kimaadili na kisiasa ya ghasia zilizopita.

Kuachiwa kwa wafuasi hao ambako kunakidhi sheria za kimataifa za haki za binadamu pia kunaenda sambamba na mapendekezo yaliyokuwa yametolewa na mtaalamu huru huyo pamoja na ripoti zingine za kitaifa, kimataifa na mashirika ya kiraia ya kimataifa.