Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu lajadili mustakhbali wa vijana na maendeleo ya milenia

Baraza Kuu lajadili mustakhbali wa vijana na maendeleo ya milenia

Mkusanyiko wa kimataifa wa vijana umefanyika leo kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ukiangazia kujenga uongozi wa vijana kwa ajili ya ufanisi wa malengo ya maendeleo ya milenia, MDGS. Joshua Mmali ana taarifa zaidi

(TAARIFA YA JOSHUA)

(WIMBO)

Wimbo, wa kijana mmoja ambaye anashiriki mkusanyiko wa leo, wenye umbo la bunge la vijana. Kauli mbiu ya mkusanyiko wa leo, ambao ni wa kumi na mbili wa aina yake, imekuwa ni “Kwenye barabara ya vitendo: Kuenda hatua zaidi ya MDGS, baada ya 2015”.

Mkusanyiko huo umehutubiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Ban Ki-Moon, Mwakilishi Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu muungano ya ustaarabu, Nassir Abdoulaziz Al-Nasser na mjumbe wa vijana katika Umoja wa Mataifa, Jane Goodall.

Katika hotuba yake, Katibu Mkuu changamoto katika dunia ya sasa ya vijana ni nyingi, na kuna kazi nyingi ya kufanya kabla ya tarehe ya mwisho ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia.

(SAUTI YA BAN)

“Viongozi wa kimataifa wana wajibu wa kuhakikisha mustakhbali wenu endelevu, lakini mna jukumu kubwa la kuchangia: Mdai uwajibikaji, mtoe ushawishi kama wapokezi wa huduma na watatathmini wa mambo, mchagize msukumo wa kasi kupitia mawazo na nguvu zenu. Mwezi ulopita, sote tulichochewa na Malala Yousafzai kwenye Umoja wa Mataifa. Tufuate mfano wake, kutetea haki na kuchukuwa hatua kuhusu tunachoamini. Tukishirikiana, tunaweza kujenga mstakbali tunaotaka.”