Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia ya kina mama wajawazito wanahitaji msaada Syria:UNFPA

Mamia ya kina mama wajawazito wanahitaji msaada Syria:UNFPA

Umoja wa Mataifa umesema kuwa umeanza kuingiwa na wasiwasi juu ya usalama wa raia Syria hasa wale walioko katika mji wa Homs ambako mapigano baina ya vikosi vya serikali na kundi la waasi yanaripotiwa kushika kasi.Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu UNFPA limesema kuwa zaidi ya raia 400,000 wameendelea kusalia njia panda kutokana na kuzongwa na mapigano hayo.

Shirika hilo linasema kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa maafa kuongezeka na lina wasiwasi wa akina mama wengi wajawazito kuwa katika hali mbaya ya kiusalama

Ili kukabiliana na hali hiyo UNFPA imetuma maafisa wake kwa ajili ya kutoa huduma za uzazi salama katika eneo la Al-Waer. Pia shirika hilo limepanga kusambaza huduma nyingine kwa ajili ya kukabiliana na mahitaji ya dharura.