Nchi zimetakiwa kuheshimu mikataba inayohusu watu wa asili:PIllay

7 Agosti 2013

Nchi zinapaswa kufanya juhudi zaidi za kuenzi na kuimarisha mikataba yao inayohusu watu wa asili, bila kujali ni lini ilitiwa saini. Hayo yamesemwa na kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay katika taarifa yake ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya watu wa asili ambayo kila mwaka hufanyika Agost 9, George Njogopa na maelezo kamili.(TAARIFA YA GEORGE NJOGOPA)

Pillay amesema kuwa, mamlaka za kidola zinawajibika kuheshimu mikataba hiyo hata kwamba ilisaidiwa karne kadhaa zilizopita.Amesema kuwa kuwepo kwa mikataba hiyo kunadhihirisha uhisiano uliopo baina ya dola na watu hao wa asili.

Ameeleza kuwa, mara zote mikataba inachukua sura muhimu ambayo inatoa kitambulisho cha kumalizika kwa migogoro na mikwaruzano iliyojitokeza katika vipindi vya nyuma.

Kwa upande mwingine, Pillay alizungumzia umuhimu wa tamko la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za msingi kwa watu wazawa lililopitishwa mwaka 2007 akisema kuwa kuwepo kumeleta matumaini kwa watu hao wazawa.

Tamko hilo pamoja na mambo mengine, linaweka zingatio maeneo yanayohusu usawa, kuheshimiwa kwa mikataba ya kimataifa inayowalenga wazawa na kutambulika uwepo wao.