Watoto zaidi waachiliwa na jeshi la Myanmar:UNICEF

7 Agosti 2013

Mratibu wa Umoja wa mataifa nchini Myanmar na shirika la kuhudumia watoto UNICEF wamekaribisha hatua ya jeshi la Myanmar la kuwaachilia watoto na vijana 68 walikuwa jeshini. Jason Nyakundi na maelezo zaidi(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Hatua hii ya leo inajiri baada ya kuachiliwa kwa watoto wengine 42 na vijana wengine wa umri mdogo mwezi mmoja uliopita wakati wa shughuli  ya kihostoria kati ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Mynmar inayolenga kuhakikisha kuwa watoto wote wameachiliwa kutoka jeshini.

Sherehe hizo zilihudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu kutoka jeshini ,waakilishi kutoka kwa wizara ya ulinzi ,ile ya masuala ya kijamii, wizara ya uhamiaji , mratibu wa Umoja wa Mataifa na UNICEF, mashirika likiwemo Shirika la kazi duniani ILO na lile la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. Bi Shalini Bahuguna ni naibu mwakilishi wa Shirika la UNICEF nchini Myanmar.

(SAUTI YA SHALINI BAHUGUNA)

Hatua ya kuachiliwa kwa wototo ni ya nne baada ya makubaliano kati ya serikali ya Myanmar na jopo la Umoja wa Mara linalohusika na kuripoti ukiukaji wa haki za watoto kuambatana na azimioa la baraza la usalama la Umoja wa Mataifa nambari 1612.