Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unesco yalaani mauaji ya mwandishi Ufilipino

Unesco yalaani mauaji ya mwandishi Ufilipino

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO Irina Bukova, amaelaani mauaji ya mwandishi, mpiga picha Mario Sy aliyepigwa risasi nyumbani kwake katika mji wa Santo Ufilipino Agosti 1

Katika taarifa yake Bi Bukova amesema inastua kuona waandishi watatu wanauwawa kwa kupishana siku mbili na kuzitaka mamlaka husika kuwafikisha wahalifu katika vyombo vya sheria.

Mwandishi huyo anakuwa watatu kuuwawa katika kipindi kifupi nchini humo baada ya Bonifacio Loreto na Richard Kho.