Kumekuwa na ongezeko kubwa la wahamiaji nchini Yemen-UNHCR

6 Agosti 2013

Kumekuwa na ongezeko kubwa la wahamiaji kutoka eneo la Pembe ya Afrika wanaomiminika nchini Yemen katika kile kinachoelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR ni kitisho kinachoendelea kusalia kwenye eneo hilo.Katika kipindi cha miezi sita iliyopita, jumla ya wakimbizi waliosajiliwa walifikia zaidi 46,000 na idadi hiyo ilitazamiwa kuongezeka kadri siku zinavyoenda.

UNHCR inasema kuwa kiwango cha watu wanaomba hifadhi,ukimbizi pamoja na wahamiaji wa kawaida nchini Yemen imeendelea kuongezeka na kuna wasiwasi idadi hiyo ikawa kubwa zaidi ya ile iliyoshuhudiw amwaka uliopita iliyokuwa 107,500.

Lakini hata hivyo shirika hilo limesema kuwa kiwango cha mwaka huu kuanzia msimu wa mwezi January hadi Juni ni ndogo ikilinganishwa na ile ya mwaka jana ya kipindi kama hicho.