Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msaada waanza kuwafikia waathirika wa mafuriko Nicaragua: WFP

Msaada waanza kuwafikia waathirika wa mafuriko Nicaragua: WFP

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP na serikali ya Nicaragua Ijumaa iliyopita wamepeleka awamu ya pili ya msaada wa chakula ili kuzisaidia familia zilizoathirika na mvua na mafuriko nchiniNicaragua.Watu wengi walioathirika na mvua na mafuriko hayo ni jamii 25 za watu wa asili kutoka kabila la Miskito wanaoishi jimbo lililojitenga la Atlantic Kaskazini la Nicaragua.