Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

China yaongoza katika matumizi ya raslimali duniani

China yaongoza katika matumizi ya raslimali duniani

Taifa la China limetajwa kupiga hatua mbele ya mataifa mengine duniani katika matumizi ya bidhaa hali ambayo imechangia kuwepa kwa changamoto za kimazingira lakini hata hivyo imesalia kuwa mtumiaji mkubwa zaidi wa raslimali dunaini. Jason Nyakundi na taarifa zaidi.

(Taarifa ya Jason)

Kulingana na ripoti mpya kutoka kwa Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP ni kwamba kuendelea kukua kwa taifa la China kumeifanya kuwa mtumiaji mkubwa wa bidhaa zikiwemo za ujenzi , makaa ya moto na chuma. Mkurugenzi mkuu wa UNEP Achim Steiner anasema kuwa China imeshuhudia ukuaji mkubwa kwa muda wa miongo kadha iliyopita hali ambayo imechangia kuwa mtumiaji mkubwa wa raslimali. Huku ukuaji huo ukiwa umewakwamua wengi kutoka kwenye umaskini umechangia pia kuwepo kwa madhara makubwa kwenye mazingira kupitia kwa matumizi ya raslimali hiyo. Ripoti hiyo inaeleza kuwa China kama moja ya mataifa yanayoinuka kichumi inahitaji kuwekeza zaidi kwenye miundo mbinu iliyo bora hasa kwenye usafiri wa umma.