Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawasiliano changamoto ya unyonyeshaji Tanzania: Dk Rashid

Mawasiliano changamoto ya unyonyeshaji Tanzania: Dk Rashid

Wakati wiki ya kimataifa ya unyonyeshaji ikiendelea, nchini Tanzania mkakati wa elimu kwa uma unakabiliwa na changamoto ya mawasiliano katika kuwafikia walengwa wakuu, ambao ni wanawake wanaonyonyesha.

Katika mahojiano maalum na idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa, naibu waziri wa wizara ya afya wa nchi hiyo Dk Seif Rashid amesema wizara ina mkakati wa kuongeza nguvu katika kutoa elimu ya afya kwa uma na kuongeza kuwa wengi wanaitikia wito wa kunyonyesha watoto kwa kuzingatia kanuni za afya.

SAUTI ( DK RASHID)

Mahojiano kamili na Naibu waziri wa wizara ya afya nchini Tanzania yatapatikana katika ukurasa wetu.