UNAMA yakaribisha uteuzi wa wajumbe wa tume huru ya Uchaguzi

5 Agosti 2013

Kamishna ya Usaidizi ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan UNAMA, umesema kuwa umepokea kwa matumaini makubwa taarifa za kuteuliwa kwa wajumbe wa tume huru ya uchaguzi na kusema kuwa na kuhaidi kuendelea kufanya nayo kazi hasa kipindi hicho ambacho taifahilolinajiandaa kwa uchaguzi mkuu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, UNAMA imesema kuwa kuteuliwa kwa wajumbe wa tume hiyo kumekuja  wakati muafaka na ni matumaini ya wengi tume hiyo itafanya kazi zake kwa weledi mkuu.

Afghanistan ambayo imekuwa ikiandamwa na matukio ya mashambulizi ya kuviziwa tangu kuangushwa kwa utawala wa Taliban, inatazamiwa kuwa na uchaguzi wake mkuu hapo mwakani 2014.

UNAMA imehaidi kuendelea kuliunga mkono taifa hilo ili kufanikisha uchaguzi huo mkuu ujao ambao unatazamiwa kubainisha mwelekeo halisi katika siku za usoni.