Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakati wa kuchukua hatua dhidi ya ukimwi ni sasa:Charlize Theron: Global Fund

Wakati wa kuchukua hatua dhidi ya ukimwi ni sasa:Charlize Theron: Global Fund

Mwanaharakati wa vita dhidi ya ukimwi na mcheza csinema maarufu Charlize Theron leo amekutana na mabalozi vijana ambao wanachukuliwa kama mfano kwa vijana wenzao na kuelimisha jinsi gain ya kuzuia kusambaa kwa virusi vya HIV katika jamii zao nchini Afrika ya Kusini.

Programu ya mabalozi vijana inawaelimisha vijana wavulana kwa wasichana wa umri wa kati ya miaka 18 na 30 kwenye jimbo la KwaZulu Natal province kusambaza ujumbe wa kupambana na HIV wakiwashirikisha vijana mashuleni ,kwenye makundi ya utoaji ushauri nasaha, makanisani, kwenye matukio ya michezo na hata kwenda nyumba kwa nyumba kukutana na watu majumbani kwao.

Mpango huo unafadhiliwa na mfuko wa kimataifa wa kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria yaani Global Fund.

Bi Theron amesema anatiwa moyo na juhudi za vijana wakitoa mchango mkubwa katika vita dhidi ya ukimwi. Afrika ya Kusini ina idadi kubwa ya watu wanaoishi na virusi vya HIV duniani huku makadirio ya sensa ya mwaka 2011 yakionyesha kwamba watu milioni 6.4 wanaishi na virusi vya HIV na milioni 2.1 kati yao wanapokea dawa za kurefusha maisha.