Katibu Mkuu Amteua Ibrahim Thiaw wa Mauriatania kama Naibu Mkurugenzi Mkuu, UNEP

2 Agosti 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amemteua Ibrahim Thiaw wa Mauritania kuwa Naibu Msaidizi wake na wakati huo huo kuwa Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shrika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEPBwana Thiaw anachukua nafasi ya Amina Mohamed wa Kenya, ambaye Ban amemshukuru kwa mchango wake na huduma kwa UNEP.

Akiwa na uzoefu wa miaka 30 katika masuala ya mazingira na maendeleo endelevu, Thiaw pia ana ujuzi kuhusu UNEP na  Kazi alizowahi kufanya  zinajumuisha ngazi ya kitaifa na kuongoza programu za kimataifa za Umoja wa Mataifa na michakato baina ya serikali mbali mbali.

Alijiunga na UNEP mwaka 2007kamaMkurugenzi kitengo cha utekelezaji wa sera za mazingira (DEPI) na kabla ya hapo alifanya kazi kwa miaka 15 katika shirikisho la Uhifadhi duniani (IUCN) ambako alishikilia nyadhifa tofauti ikiwemo  Kaimu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi eneo la Afrika Magharibi. Bwana Thiaw alianza kazi yake nchiniMauritaniaalikozaliwa na ambako alihudumukamaWaziri wa maendeleo ya vijijini kwa muda wa miaka kumi.