Maelfu ya watoto wakimbia ghasia mashariki mwa DRC na kuingia Uganda:UNICEF

2 Agosti 2013

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa maelfu ya watoto wamekimbia ghasia ambazo zimeshuhudiwa hivi majuzi karibu na mji wa Kamango mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC .Jason Nyakundi na taarifa zaidi. (PKG YA JASON NYAKUNDI)

UNICEF inasema kuwa zaidi ya watoto 37,000 wamekimbilia usalama upande wa mpaka wa Uganda ambapo hali ya kibinadamu kwa wale waliokimbia majuzi ikiwa ni mbaya.

Shirika la UNICEF linasema kuwa karibu watoto 122 wametambuliwa kuwa wasio na wazazi waliotenganishwa na familia zao lakini hata hivyo hakuna ripoti za watoto waliouawa au kujeruhiwa kutokana na ghasia hizo zilizotolewa.

Kwa sasa UNICEF imetoa ombi la dola milioni saba ambazo zitatumiwa kugharamia huduma kwa watoto nchini Uganda hadi mwishoni mwa mwaka huu. Patrick McCormick ni msemaji wa UNICEF mjini Geneva.

 (CLIP YA PATRICK McCORMICK)

Wengi wa watoto hawa wakimbizi wameshuhudia visa vya uvamizi usiku wa manane  hali inayozua hofu na kusababisha watu wa familia kukimbilia pande tofauti ili wasiuawe. Baadhi ya watoto walitenganishwa na wazazi na ndugu zao wakati  huo na wakasafiri peke yao kwenda kwa mpaka wa Uganda.”

 UNICEF inazitaka pande zote husika kuhakikisha kuwa watoto wamelindwa.